Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dr. Mariam al-Sadiq al-Mahdi amesema kuwa, anatoa wito wa kusitishwa uadui dhidi ya Sudan unaofanyika kwa maslafi binafsi ya kundi fulani la watu.
Kadhalika amesema kuwa, kila mara Ethiopia inapokabiliwa na matatizo ya ndani huinyooshea kidole Sudan na kuionyesha kuwa ni msababishaji wa matatizo hayo hali ya kuwa si kweli.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Sudan ameitahadharisha Ethiopia na kuitaka iachane na sera zake za kuendesha uadui dhidi ya Sudan.
Wasiwasi katika mpaka wa Sudan na Ethiopia uliongezeka baada ya kutokea mapigano katika eneo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana (2020). Zaidi ya wakimbizi 50 elfu wa Ethiopia walikimbilia katika maeneo ya mashariki mwa Sudan kukwepa mapigano hayo.
Ugomvi baina ya Sudan na Ethipia unahusiana na maeneo ya kilimo katika eneo la al Fushqa hasa baada ya wakulima kutoka Ethiopia kuyavamia maeneo hayo ya Sudan.
Hivi karibuni kuliripotiwa kutokea mapigano ya silaha baina ya wanajeshi wa Sudan na Ethiopia huku kila upande ukiushutumu upande mwingine kuwa ndio ulioanzisha mapigano hayo. Hivi karibuni pia nchi hizo mbili zilifanya mazungumzo mjini Khartoum kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
342/