Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kesho Alkhamisi ataelekea Dushanbe kwa mwaliko rasmi wa Rais Emomali Rahmonov wa Tajikistan na kwa lengo la kushiriki kikao cha wakuu wa Jumuiya ya Shanghai.
Ziara ya Rais Ebrahim Raisi nchini Tajikistan itakuwa ya kwanza nje ya nje kama Rais wa Jamhuri ya Kiislamu kufuatia mwaliko rasmi wa mwenzake wa nchi hiyo na kwa ajili ya kushiriki na kuhutubia kkao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.
Katika ziara yake ya kesho nchiini Tajikistan, Rais wa Iran mbali ya kushiriki katika kikao hicho cha Jumuiya ya Shanghai atafanya mazungumzo ya pande mbili na wakuu na marais wa jumbe shiriki katika kikao hicho.
Rais Ebrahim Raisi anafutana na ujumbe wa ngazi ya juu wa maafisa wa kisiasa na kiuchumi wa Iran katika safari hiyo huko Tajikistan.
Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai iliasisiwa mwaka 2001 kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na vitendo vya uchupaji mipaka na kuimarisha ushirikiana wa kiuchumi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni wanachama watazamaji katika jumuiya hiyo.
342/