Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ripoti yake hiyo ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa umesema pia kuwa, mamluki wanaodhaminiwa kifedha na Imarati nchini Libya ndicho chanzo kikuu cha kifedha za magenge mengi yenye silaha kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan.
Katika ripoti yao hiyo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa, awali misaada ya kifedha ya Umoja wa Falme za Kiarabu ilikuwa inatumwa kwa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar. Hivi sasa Imarati inalitumia kundi hilo kuyafikishia fedha magenge yenye silaha ya magharibi mwa Sudan.
342/