12 Aprili 2022 - 17:40
Duru ya pili ya uchaguzi Ufaransa; mchuano baina ya Macron na Le Pen

Uchaguzi wa Rais nchini Ufaransa umemalizika huku Emmanuel Macron na Marine Le Pen wakiingia katika duru ya pili. Kwa utaratibu huo, siku 14 zijazo yaani tarehe 24 mwezi huu hatima ya uchaguzi huo itajulikana na mshindi wa duru hiyo atapata tiketi ya kuingia katika ikulu ya Elizeh.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanaonyesha kuwa, Macron amepata asilimia 28.5 ya kuwa na Le Pen asilimia 24.4 na hivyo kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi. Wagombea 12 kutoka vyama mbalimbali wameshiriki katika duru hiyo ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa huku washindani wakuu wakiwa ni Macron na Le Pen. Wanasiasa hao wawili sasa wameingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyopangwa kufanyika tarehe 24 ya mwezi huu wa Aprili; na ni wazi kuwa siku zijazo zitakuwa siku muhimu za maamuzi kwa mustakabali wa kisiasa na kiuchumi wa Ufaransa na Umoja wa Ulaya.   

342/