15 Aprili 2022 - 13:15
Macron apinga madai ya kufanyika mauaji ya halaiki nchini Ukraine

Katika mazungumzo yake na Rais wa Ukraine, Rais wa Ufaransa ameelezea upinzani wake dhidi ya matumizi ya neno mauaji ya kimbari kuhusiana na matukio ya Ukraine.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameyasema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelinskyy.

Macron amekiambia kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kwamba: "Sambamba na kuheshimu yanayojiri nchini Ukraine lakini ninapinga matumizi ya neno 'mauaji ya kimbari'."

Amesema: "Nilimpa (Zelenskyy) jibu la moja kwa moja, nikisema kwamba wanasheria, sio wanasiasa, ndio wanaopaswa kuamua ikiwa neno mauaji ya kimbari linaweza kutumika kuhusu vita vya Ukraine au la. 

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne iliyopita alimtuhumu Rais Vadimir Putin wa Russia kuwa amefanya mauaji ya kimbari nchini Ukraine. Hata hivyo White House ilisema baadaye kwamba matamshi hayo ya Biden ni mtazamo wake binafsi na si msimamo rasmi wa serikali ya Washington. 

Kufuatia operesheni ya kijeshi ya Russia dhidi ya Ukraine iliyoanza Februari 24 , kambi ya Magharibi ikiongozwa na Marekani imeiwekea Moscow vikwazo vikali vya kiuchumi, ambavyo hata hivyo vimekuwa na taathira hasi pia kwa chumi za Wamagharibi wenyewe.

342/