Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa Jumatano usiku, wizara hiyo imesema majasusi hao wa Mossad wanahusika katika kusambaza taarifa na nyaraka za siri.
Majasusi hao wamekamatwa kufuatia amri ya mahakama lakini bado uraia wao haujatajwa.
Mwezi Julai mwaka jana Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ujasusi cha wizara hiyo alisema vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu viliwatia nguvuni magaidi hao waliojipenyeza nchini kupitia mpaka wa magharibi.
Alieleza bayana kuwa, mbali na kukamatwa maajenti hao wa Mossad, lakini maafisa usalama nchini walifanikiwa pia kunasa idadi kubwa ya silaha na mada za miripuko zilizoingizwa nchini kimagendo na magaidi hao wenye mfungamano na Wazayuni.
Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Wizara ya Intelijensia ya Iran alisema majasusi hao wa Mossad ya Israel walitiwa mbaroni kutokana na kuwa macho vyombo vya usalama vya taifa hili.
342/