ofisi ya Ayatullah Rouhani imetoa tangazo ikieleza kwamba: Magharibi ya Ijumaa ya jana, Desemba 16, 2022, roho tukufu na iliyotukuka ya Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani imeungana na mababu zake watoharifu.Alimu huyo alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Ayatullahil-Udhma Khoui (RahamtuLlahi-Alayhi) na alifikia daraja ya kielimu ya Ijtihad akiwa na umri wa miaka 14 kwa kuthibitishwa kimaandishi ya walimu wake.Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani amealifu vitabu kadha wa kadha kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi, mojawapo ya vilivyo muhimu zaidi kikiwa ni kitabu kiitwacho Fiqhu-Sadiq.Mwanazuoni huyo alizaliwa katika mwezi wa Mfunguo Nne, Muharram 1345 mwaka wa mwandamo wa Hijria katika mji mtukufu wa Qom.../
342/