Kwa mujibu wa televisheni ya Bloomberg, nchi za Ulaya zimepata hasara hiyo ya dola trilioni moja kutokana na mgogoro wa nishati na kuacha kwao kutumia gesi ya Russia na pia kutokana na hatua ya nchi hizo ya kuiwekea vikwazo Moscow.
Televisheni hiyo imeripoti pia kuwa, sababu ya hasara hiyo kubwa ziliyopata nchi za Ulaya ni kupaa bei ya umeme ya mashirika ya uzalishaji bidhaa pamoja na kupanga gharama za bidhaa hizo kwa watumiaji.
Televisheni hiyo ya nchini Marekani vile vile imetabiri kuwa, huu ni mwanzo tu wa mgogoro mkubwa wa nishati uliozikumba nchi za Ulaya na Magharibi. Mgogoro mkubwa kiasi hicho haujawahi kuzikumba nchi hizo katika kipindi cha miongo mingi iliyopita.
Televisheni hiyo yenye makao makuu yake mjini New York Marekani pia imesema, baada ya msimu wa baridi kali, akiba ya gesi ya nchi za Ulaya itakauka kabisa na kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa zaidi hasa kwa kuzingatia kuwa nchi hizo hivi sasa zinapokea kiwango cha chini kabisa cha gesi ya Russia.
Wachambuzi na wataalamu waliopewa nafasi ya kutoa maoni yao na televisheni hiyo pia wamesema kuwa mgogoro wa nishati barani Ulaya utaendelea kwa uchache hadi mwaka 2026 wakati nchi kama Qatar na Marekani zitakapoweza kuongeza kiwango cha uzalishaji wao wa gesi na kuifikisha kwa nchi za Ulaya.
342/