Akizungumza katika hafla ya kuanza vikao vya bunge la taifa la nchi hiyo (AN) katika mwaka 2023-2024, Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amekosoa jitihada za Marekani za kutoa pigo kwa nchi hiyo kupitia kuasisi taasisi zilizo dhidi ya serikali halali ya Caracas na kuongeza kuwa, siasa za Kitrump dhidi ya Venezuela za kushambulia na kuiondoa mihimili mitatu ya dola kwa kumteuwa rais wamtakaye, bunge la taifa na idara ya mahakama zimefeli kutoka nje.
Rais Maduro ameongeza kuwa sera za Marekani mkabala wa uhakika wa uwezo wa kiutendaji wa taasisi za kidemokrasia za Venezuela zimegonga mwamba. Wakati huo huo Maduro amezitaka Marekani na wale wote wanaopinga serikali anayoiongoza kuacha kuingilia haki za wananchi wa Venezuela kwa kuiba rasilimali za nchi hiyo kupitia taasisi zao za uongo.
Shughuli za ubalozi wa Venezuela nchini Marekani ambao ulikuwa chini ya udhibiti Juan Guaido kiongozi wa upinzani nchini Venezuela zimesimamishwa baada ya kuvunjwa serikali hiyo ya mpito. Aidha wabunge wa zamani wa bunge la taifa la Venezuela wameafiki kuvunjwa kwa serikali hiyo ya muda iliyokuwa ikiongozwa na Juan Guaido.
Mwezi Januari mwaka 2019 Guaido alijitangaza kuwa rais wa serikali ya mpito ya Venezuela kwa kuungwa mkono na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na nchi za Magharibi na kisha msururu wa vikwazo dhidi ya Venezuela ukaanza kwa lengo la kuing'oa madarakani serikali ya Maduro.
Vyombo vya habari vimekutaja kuvunjwa serikali hiyo ya mpito ya Venezuela na pia kuondolewa Guaido katika nafasi ya kiongozi wa upinzani kuwa sawa na kukiri kushindwa mrengo wa kushoto na kuibuka na ushindi Rais Nicolas Maduro.
342/