19 Februari 2023 - 14:13
Ebrahim Raisi: Taifa la Iran limesambaratisha njama za maadui kwa 'istiqama' ya kupigiwa mfano

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa la Iran limefanikiwa kusambaratisha njama za maadui kwa muqawama na istiqama ya kupigiwa mfano.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo wakati viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mabalozi na wawakilishi wa nchi za Kiislamu pamoja na wageni walioshiriki kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, walipoonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumamosi, kwa mnasaba sikukukuu ya Mab'ath na ya kupewa Utume Mtume wetu Muhammad SAW.  Aidha ametumia fursa ya hotuba hiyo fupi kuwashukuru wananchi wa Iran kwa kufanya hamasa nyingine kubwa ya kusambaratisha njama za adui, wakati wa matembezi ya kuadhimishwa mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Rais Ebrahim Raisi amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadui kama ilivyokuwa katika zama za mwanzoni mwa Uislamu, walianza kulivamia taifa la Iran kwa vita vya kijeshi, kiuchumi, kisiasa na kipropaganda. Lakini kwa mahesabu yao mabovu na ghalati kuhusu taifa la Iran, muda wote njama zao maadui zinafeli. 

Vile vile amesema, hadi jana Wamagharibi walikuwa wanadai kuwa wanataka kufikia makubaliano na Iran, lakini wakati walipoona hawawezi kukabiliana na matakwa ya haki ya wananchi wa Iran, walizusha fujo humu nchini ili wapate kisingizio cha kutoka kwenye mazungumzo.

Jana Jumamosi, viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wawakilishi na mabalozi wa nchi za Kiislamu pamoja na wageni walioshiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu walikutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa Sambamba na maadhimisho ya sikukuu tukufu ya kubaathiwa na kupewa Utume Bwana wetu Muhammad SAW hapa jijini Tehran.

342/