9 Machi 2023 - 19:41
Arab League yaitaka jamii ya kimataifa kusitisha mauaji ya Israel huko Jenin

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imeitaka jamii ya kimataifa kusitisha mauaji na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina hususan katika eneo la Jenin.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu sambamba na kulaani vikali jinai mpya zinazofanywa na Wazayuni huko Jenin, imeiomba jamii ya kimataifa, hasa Baraza la Usalama, kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kukomesha jinai zinazofanyika katika miji na vijiji mbalimbali vya Palestina.

Taarifa hiyo imesema: Mauaji ya umwagaji damu ya Jenin ni jinai kubwa ya nne ya iyofanywa na utawala huo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023 katika fremu ya vita vya wazi vya serikali ya mrengo mkali wa kulia na mawaziri wabaguzi wa utawala wa Kizayuni. 

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu pia imelaani mashambulizi ya mara kwa mara ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na kuvunjiwa heshima eneo hilo takatifu, ambavyo vinafanywa kwa msaada na himaya ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imesema baraza la mawaziri la serikali ya Israel linapaswa kuwajibishwa kutokana na jinai za kupangwa zinazofanyika dhidi ya Wapalestina na matokeo yake.

Jumanne iliyopita wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walishambulia mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuua Wapalestina wasiopungua 6.

Idadi kubwa ya askari wa kikosi maalumu cha jeshi la utawala haramu wa Israel ilivamia mji wa Jenin na kambi za wakimbizi na kukabiliwa na mapambano makali Wpalestina. Hujuma hiyo imefanyika sambamba na mashambulizi mengine ya jeshi la Israel katika mji wa Nablus. 

Kushika hatamu za uongozi serikali yenye siasa kali za mrengo wa kulia huko Israel yenye mawaziri wenye misimamo mikali kama "Itamar Ben Goyer" Waziri wa Usalama wa Ndani na "Bezalel Smotrich" Waziri wa Fedha katika baraza la mawaziri la Netanyahu, ambaye ametoa wito wa kufutwa kikamilifu kitongoji cha Wapalestina cha Huwara kusini mwa Nablus kumezidisha jinai za utawala huo haramu dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.

342/