Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika hayo katika ukurasa wake wa Twitter kufuatia machafuko makubwa na maandamano yanayoendelea kufanywa na wananchi wa Ufaransa kupinga mageuzi ya pensheni ambayo yanaongeza umri wa kustaafu kwa miaka miwili hadi 64. Kan'ani amesema: Imeripotiwa katika habari kwamba waandamanaji wa Ufaransa wamechoma moto "Manispaa ya Bordeaux" na kwamba wazima moto wamejiunga na waandamanaji.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa Tehran haiungi mkono uharibifu na machafuko, lakini inasisitiza kuwa badala ya kuibua machafuko katika nchi nyingine, Paris inapaswa kusikiliza sauti ya watu wake na iepuke kufanya ukatili dhidi yao.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, serikali ya Ufaransa inapaswa kuzungumza na watu wake na kusikiliza sauti zao. Ukatili wa aina hii hauoani na mienendo ya kukaa kwenye kiti cha kutoa somo la maadili na kuyahubiria mataifa na nchi nyingine.
Maandamano ya Wafaransa kupinga sheria ya pensheniNasser Kan'ani amesisitiza kuwa waandamanaji wa Ufaransa wanasubiri kuona mkanda wa video wa mawaziri wa kike wa Ulaya, Australia na Canada wakiwaunga mkono wanawake wa Ufaransa wanaoandamana.
Ikumbukwe kuwa Alkhamisi ya wiki iliyopita Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alilipiga chenga Bunge la nchi hiyo na kutumia mamlaka maalumu ya kikatiba kulazimisha mageuzi ya pensheni ambayo yanaongeza umri wa kustaafu kwa miaka miwili hadi 64.
Kabla ya kulikwepa Bunge, Rais wa Ufaransa alikuwa ametishia kwamba ataivunjilia mbali taasisi hiyo ya kutunga sheria iwapo haitapasisha muswada tata wa kuongeza umri wa kustaafu.
Kwa mujibu wa mpango huo, umri wa kustaafu nchini Ufaransa umeongezeka kutoka miaka 62 hadi 62. Marekebisho hayo ya umri wa wastaafu yamepingwa vikali na wananchi vyama vya wafanyakazi.
342/