29 Julai 2023 - 20:20
Korea Kaskazini yaahidi kuendeleza uhusiano na China

Akizungumza na ujumbe wa China ulioitembelea Pyongyang; Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un ameahidi kuboresha zaidi uhusiano kati ya nchi mbili hizo.

Ujumbe wa maafisa wa China unaoongozwa na mjumbe wa kitengo cha kisiasa cha Chama cha Kikomonisti cha nchi hiyo, Li Hongzhong jana waliutembelea mji mkuu wa Korea Kaskazini katika kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 70 baada ya kumalizika vita vya Korea. Ujumbe huo wa China ni wa kwanza  kufanya ziara mjini Pyongyang tangu dunia iathiriwe na janga la maambukizi ya Corona. 

Mapema jana maafisa wa China na Russia walisimama bega kwa bega na kiongozi wa Korea ya Kaskazini katika gwaride la kijeshi huko Pyongyang. Ujumbe wa Russia uliongozwa na Sergei Shoigu Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo. 

Kiongozi wa Korea Kaskazini pia alimtembeza Shoigu katika maghala ya silaha ya nchi hiyo ikiwemo kombora la balistiki la masafa marefu huko Hwasong ambalo lilifanyiwa majaribio kwa mafanikio mwezi Aprili mwaka huu.

Hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na Waziri wa Ulinzi wa Russia huko Korea ya Kaskazini tangu kusambaratika Umoja wa Kisovieti.

342/