Mnamo Januari 2018, Marekani ilikata msaada wake wa dola milioni 300 kwa shirika la UNRWA kwa lengo ya kuwashinikiza Wapalestina waukubali mpango wa mapatano wa kihaini uliopewa jina la Muamala wa Karne.Kwa mujibu wa shirika la habari la SAMA, Adnan Abu Husna, mshauri wa vyombo vya habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), amesema, "tunakabiliwa na punguzo la misaada ya kimataifa, ambayo imeathiri si Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP pekee, lakini mashirika yote ya kimataifa."Abu Husna amesisitiza kuwa UNRWA inatoa msaada wa chakula na pesa taslimu kwa Wapalestina 1,700,000 wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na Syria. Shirika hilo hutoa msaada wa chakula kwa mpangilio maalumu kwa wakimbizi 1,200,000 wa Ukanda wa Gaza. Iwapo misaada hiyo itasitishwa, -na uwezekano ni mkubwa-, Gaza itakabiliwa na baa halisi la njaa katika miezi ijayo.
342/