14 Oktoba 2023 - 20:06
UNRWA yatahadharisha: Roho za watu zitateketea endapo fueli na maji ya kunywa hayataingizwa Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa mwito wa indhari likisema: "tunataka misaada ya kibinadamu iingizwe; ikiwa fuei haitafikishwa sasa hivi Ukanda wa Gaza na kama maji ya kunywa hayatapatikana, watu wa Gaza watafariki dunia".

Kwa mujibu wa Al-Jazeera, UNRWA imebainisha kuwa: karibu watu milioni moja wameyahama makazi yao huko Ukanda wa Gaza ndani ya muda wiki moja. Kwa upande mwingine, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF amesisitizia ulazima wa kuwalinda watoto kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kibinadamu na kutangaza kuwa: hali ya kibinadamu Gaza ni ya janga na maafa hasa kwa watoto na kwwamba zaidi ya watoto 700 wamepoteza maisha katika eneo hilo tangu yalipoanza mashambulizi ya Israel. Msemaji wa UNICEF ameendelea kueleza kuwa: hakuna mahali popote palipo salama kwa watoto katika Ukanda wa Gaza, na hakuna maji, chakula wala dawa.Wakati huohuo Shirika la Afya Duniani WHO limetahadharisha kuhusu kusambaratika kwa mfumo wa afya wa Gaza na kueleza kuwa: "hospitali za Gaza zimebakiwa na umeme wa  saa chache tu na kulazimika kutumia majenereta ya umeme. Hali itakuwa mbaya zaidi akiba ya mafuta itakapokwisha, na matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi na zaidi kwa wagonjwa, hasa kwa majeruhi wanaohitaji upasuaji na wagonjwa wa kitengo cha wagonjwa mahututi.

 Wakati huo huo, Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa hali ni mbaya sana katika hospitali za Gaza na kuna hitajio la dharura la wafanyakazi wa kitengo cha tiba. Katika kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, wapiganaji wa Muqawama wa Palestina Jumamosi iliyopita walianzisha operesheni iliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa ambayo hadi sasa imeshaangamiza Wazayuni wasiopungua 1,500. Kufuatia operesheni hiyo ya Muqawama wa Palestina, baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni lilitangaza hali ya vita na kuchukua hatua ya kukata maji na umeme katika Ukanda wa Gaza. Sambamba na hatua hiyo, jeshi la utawala haramu wa Kizayuni limefanya mashambulio ya kinyama ambayo yamelenga vituo vingi vya raia, zikiwemo hospitali kadhaa, misikiti na majengo ya makazi katika Ukanda wa Gaza. Hadi sasa Wapalestina wasiopunguia 2,200, wakiwemo mamia ya wanawake na watoto wameshauawa shahidi katika mashambulizi hayo ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda huo.../


342/