29 Oktoba 2023 - 14:30
Kim atabiri: Mashambulio ya Israel yanaandaa mazingira ya kuzuka Vita vya Tatu vya Dunia

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema, mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina yanaandaa mazingira ya kuzuka Vita vya Tatu vya Dunia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Kim ameyasema hayo alipobainisha misimamo yake kuhusu matukio ya hivi karibuni katika Mashariki ya Kati na kusisitiza kwamba Vita vya Tatu vya Dunia vinakaribia kutokea. Akizungumzia mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema, "mapigano katika Mashariki ya Kati yataishia kwenye Vita vya Tatu vya Dunia, na vita hivi vinakaribia kuanza. Inapasa kila mtu ajiweke tayari."Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kim Jong Un ameeleza kwamba, mapigano hayo yatasababisha uhasama ambao unaweza kuenea katika maeneo mengine ya dunia.

 Vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza vimeingia katika siku ya 23 tangu ilipoanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya wanamuqawama wa Palestina. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, idadi ya watoto Wapalestina waliouawa shahidi kutokana na mashambulio ya kinyama ya jeshi la Israel ilifikia 3,595 hapo jana.../


342/