Lazzarini amesema hayo kwa mnasaba wa kupita siku 100 tangu Israel ianze kuwashambulia wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa mabomu, mizinga na ndege za kivita akisisitiza kwamba, Wapalestina wamelazimika kuyahama makazi yao kwa wingi zaidi tangu mwaka 1948 kutokana na mashambulizi hayo. Lazzarini ameongeza kuwa "watu milioni 1.4 wamekimbilia kwenye vituo vya UNRWA na wanalazimishwa kuishi katika mazingira yasiyo ya binadamu."
Aisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema: "Katika muda wa siku 100 zilizopita, Gaza imeshuhudia “sura mbaya ya mauti, uharibifu, kulazimishwa watu kuwa wakimbizi, njaa, hasara na mateso ambavyo vinatia doa ubinadamu wetu.”Amesema kwamba "siku 100 zilizopita ni kama miaka 100 kwa wakazi wa Gaza," na kuongeza kwamba, watu wengi wa Gaza watakuwa na majeraha ya kimwili na kisaikolojia ya kudumu katika maisha yao yote kutokana na mashambulizi ya Israel. Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefikia 23,708 na idadi ya majeruhi ni 60,500.
342/