Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili, Mufti wa Oman amesema hayo katika ujumbe wake wenye lugha kali kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu ambazo hazifanyi lolote kuvunja mzingiro wa Gaza, na amekosoa vikali misaada ya nchi hizo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mufti Al-Khalili wa Oman ambaye anajulikana kwa uungaji mkono wake kwa kadhia ya Palestina amesema: "Hali ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu imezidi kuwa mbaya na ukandamizaji umefikia kiwango cha juu kabisa." Wakati watu wanaodhulumiwa na wanaopigana wa Palestina wanateseka na njaa, jamaa zao na ndugu zao (nchi za Kiarabu) wanamsaidia adui Israeli]."
Huku akiashiria kuwa, malori ya misaada ya nchi za Kiarabu yanausaidia utawala wa Kizayuni amesema kuwa, wazee, wanawake na mayatima wa Palestina hawana chakula na hawawezi kufunika miili yao katika baridi kali ya msimu huu wa baridi. Undugu wenu wa Kiislamu, fahari ya Kiarabu na misaada ya kibinadamu imekwenda wapi? Mufti wa Oman sambamba na kuashiria kuwa, ujumbe wake unawalenga Waislamu wenye ghera na shupavu, amesisitiza kuwa, jinai za utawala haramu wa Israel zimefikia hatua mbaya kabisa na wananchi wa Palestina wamezingirwa kila upande.
342/