Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, UNRWA imesema kwamba "watoto katika Ukanda wa Gaza wanakufa polepole mbele ya macho ya ulimwengu."
Kauli hiyo umetolewa kufuatia vifo vya watoto 15 wa Kipalestina vilivyotokana na upungufu wa maji mwilini na utapiamlo katika Hospitali ya Kamal Adwan, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Jumapili iliyopita pia, Ashraf al-Qidra, msemaji wa Wizara ya Afya huko Gaza, alielezea wasiwasi wake juu ya "maisha ya watoto 6 (wengine) wanaosumbuliwa na utapiamlo na kuhara katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na kusitishwa jenereta ya umeme, mitambo ya oksijeni na udhaifu wa huduma za matibabu."
Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, Israel imeweka "mzingiro kamili" dhidi ya Ukanda wa Gaza na kukata umeme, chakula na maji kwa Wapalestina zaidi ya milioni mbili wanaoishi katika eneo hilo.
Jumapili iliyopita pia Umoja wa Mataifa ulionya kwamba vifo vya watoto "vitaongezeka sana" huko Gaza ikiwa misaada ya kibinadamu haitaongezeka haraka iwezekanavyo.
342/