Tukio hilo la ufunguzi wa Msikiti limehudhuriwa na Masheikh mbalimbali akiwemo Naibu Kadhi Sheikh Ali Ngeruko, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam, Sheikh Walid Al-Had, Sheikh Hussein Nurdin Shadhil, Maulana Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Rajab Shaban (Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Nchini Iran), pamoja na waheshimiwa Masheikh wengine wa Madh-habu ya Shia Ithna Ashari na Ahlul-Sunna Wal- Jamaa.
Aidha, wageni wengine wa Heshima waliohudhuria katika ufunguzi wa Msikiti huo ni:
1_Balozi wa Iran Nchini Tanzania, Mheshimiwa Al-Vandi.
2_Na Rais wa Jamiatul Mustafa nchini Tanzania, Dar-es-salaam, Dkt.Sheikh Ali Taqavi.
Mwenyeji wa hafla hii Tukufu ya Ufunguzi wa Msikiti alikuwa ni:
Samahat Sheikh Musabaha Mapinda.
Msikiti sio tu kwamba ni sababu ya kuzuia Mtu wa Msikiti (yaani: Mtu yule anayefungamanisha Maisha yake na Msikiti) kuingia motoni, lakini pia Msikiti ni kwa ajili ya kuwatakasa na kuwasafisha Waja wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutoka na (dhambi na Maasi), na hilo ni la thamani ya juu zaidi ya kuingia Peponi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema akimwambia Mtume wake Muhammad (s.a.w.w):
{لَمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَنْ تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَنْ يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ}
"Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanao penda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao jitakasa"
[Surat al-Tawba: Aya ya 108].