Katika taarifa yake hiyo, Hamas imelaani hujuma na mashambulio ya kikatili yanayofanywa na utawala wa Kizayuni na mauaji ya kutisha dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na njama za kichokozi unazoendeleza katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
"Tunautolea mwito umma wa mataifa yetu ya Kiarabu na Kiislamu, watetezi wa uhuru duniani, na wale wote wanaopigania haki na uhuru kuzidisha mashinikizo kwa utawala ghasibu ili ukomeshe mashambulizi yake", imeeleza sehemu moja ya taarifa hiyo ya Hamas.
Aidha, harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina imewataka walimwengu wapinge uhalifu na mipango ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Palestina, watu wake na maeneo yake matakatifu, na kulaani uungaji mkono wa Marekani kwa ukatili unaofanywa na utawala huo ghasibu.
Hamas imesema, kila njia inayowezekana lazima itumike ili kuvunja mzingiro, kukomesha mauaji, na kuhitimisha mateso ya kuwaweka Wapalestina na njaa.
Taarifa ya Hamas imemalizia kwa kusema: "tunatoa wito kwa viongozi wa dunia watekeleze jukumu lao la kihistoria katika wakati huu muhimu ambapo adui Mzayuni anaendelea kufanya jinai mbaya zaidi. Lazima wachukue hatua madhubuti kusimamisha vita hivi".../
342/
Your Comment