24 Mei 2025 - 15:30
Sheikh Zakzaky amekutana na wanafunzi wa programu ya Hifdhi ya Qur’an wa Fudiyyah kabla ya sherehe za kuhitimu

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Sayed Ibraheem Zakzaky, amekutana na wanafunzi wa Fudiyyah waliokamilisha Hifdhi ya Qur’an kabla ya sherehe za kuhitimu

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Syed Ibraheem Zakzaky, alikutana na kundi la wanafunzi wa Fudiyyah waliokamilisha masomo yao ya kusoma na kuhifadhi Qur’an Tukufu kabla ya sherehe zao za kuhitimu.

Kulingana na “Tovuti Rasmi ya Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria”, Sheikh Zakzaky alitoa hotuba yake kwa wapenzi hao wa Qur'an Tukufu akiwa katika makazi yake yaliyopo Abuja.

Katika hotuba yake kuhusu umuhimu wa kujifunza Qur’an, alifafanua kuhusu shahada ya Imam wa nane, Imam Ridha (a.s), akizingatia kuwa mwezi huu ni wa kumbukumbu ya shahada yake kupitia mkono wa watawala waovu wa wakati wake.

Mwisho wa hotuba yake, kiongozi huyo aliwahimiza wanafunzi wajitahidi zaidi katika kuunganisha maarifa waliyojifunza katika Qur’an Tukufu na vitendo vyao vya kila siku.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha