25 Agosti 2025 - 10:03
Bi. Amina Mkumba Ateuliwa Kugombea Ubunge Jimbo la Kibiti Kupitia CCM

JMAT: "Tunamtakia Bi. Amina Mkumba mafanikio mema katika kuipeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Kibiti na tunaamini ataendelea kuwa mfano bora wa uongozi wenye misingi ya maridhiano, mshikamano na amani"

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Tanzania - Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imetoa pongezi kwa Bi. Amina Mkumba, Mjumbe wa Kamati Kuu ya JMAT, kufuatia uteuzi wake kugombea Ubunge wa Jimbo la Kibiti katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025 kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Bi. Amina Mkumba ni sehemu ya familia ya JMAT na mchango wake katika shughuli za kijamii na kidini umekuwa chachu kubwa ya mshikamano na maendeleo ya kijamii katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika salamu zake za pongezi, JMAT-TAIFA imesisitiza kuwa uteuzi huu ni heshima kwa taasisi na pia ni uthibitisho wa nafasi muhimu ya wanawake katika uongozi na siasa za Tanzania.

"Tunamtakia Bi. Amina Mkumba mafanikio mema katika kuipeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Kibiti na tunaamini ataendelea kuwa mfano bora wa uongozi wenye misingi ya maridhiano, mshikamano na amani," imesema JMAT-TAIFA katika taarifa yake.

Your Comment

You are replying to: .
captcha