Kulingana na shirika la habari la Abna, shirika la habari la Saba la Yemen, likinukuu vyanzo vya usalama, liliripoti kuwa maafisa wa Imarati walioko Shabwa na Al-Riyan nchini Yemen wameelekea Ukanda wa Gaza kwa ajili ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni.
Kulingana na ripoti hii, maafisa hao wa Imarati wana jukumu la kutoa mafunzo kwa mamluki wanaohusishwa na utawala wa Kizayuni kwa kipindi cha siku 45, kuhusu jinsi ya kutumia vifaa vya kisasa vya kivita.
Vyanzo hivyo vilifafanua kuwa miongoni mwa maafisa hao wa Imarati, kuna wale ambao pia wanafanya kazi katika Hilali Nyekundu ya Imarati (Emirates Red Crescent). Ujumbe wao ni sawa na ule wanaofanya nchini Yemen katika kuwaandaa mamluki.
Walieleza kuwa mamluki wanaohusishwa na utawala wa Kizayuni wanatarajiwa kuunda vikundi mbalimbali ili kushiriki katika vita dhidi ya vikosi vya mapambano vya Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Your Comment