18 Novemba 2025 - 11:43
Source: ABNA
Waziri wa Kizayuni: Tumemtayarishia Mahamud Abbas Chumba cha Selo

Licha ya kujisalimisha kwa Mamlaka ya Palestina kwa utawala wa Kizayuni, Itamar Ben-Gvir alitaka maafisa wakuu wa mamlaka hiyo waangamizwe.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Abna, Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, alisema akimzungumzia Netanyahu: "Lazima utangaze kwamba Mahmoud Abbas (Rais wa Mamlaka ya Palestina) hana kinga."

Aliongeza: "Ikiwa watafanya hatua yoyote kuelekea kutambuliwa kwa nchi ya Palestina katika ulimwengu, na ikiwa Umoja wa Mataifa utafanya hivyo, Netanyahu anapaswa kutoa amri ya kuwaua maafisa wakuu wa Mamlaka ya Palestina."

Ben-Gvir alisema: "Mahmoud Abbas pia anapaswa kukamatwa. Tumemtayarishia selo katika gereza la Ktzi'ot."

Hii inakuja wakati ambapo Mamlaka ya Palestina inachukuliwa kuwa kibaraka wa utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi na inashirikiana kikamilifu katika masuala ya kiusalama na kijasusi na Tel Aviv.

Your Comment

You are replying to: .
captcha