Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (ABNA)- Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), Hussein Jaberi Ansari, amesema kuwa suala la Iran limevuka mipaka ya mgawanyiko wa kawaida wa kisiasa na sasa linaangaliwa kwa mtazamo wa maslahi ya juu ya taifa, huku watu wengi wakitanguliza maslahi hayo kuliko tofauti zao za awali.
Katika mkutano uliowakutanisha Mkurugenzi Mkuu wa IRNA, Hussein Jaberi Ansari, na Mhariri Mkuu wa gazeti la Kihan la Iran, Hussein Shariatmadari, pande hizo zilijadili kwa kina vipengele mbalimbali vya uimara wa Iran katika kukabiliana na changamoto za sasa, pamoja na uwezo wake wa kujizuia dhidi ya vitisho na hali halisi ya mvutano kati ya Iran na Marekani.
Jaberi Ansari alieleza kuwa Iran imefanikiwa kujenga mfumo wa kina wa kujihami na kujizuia dhidi ya vitisho unaojumuisha nyanja mbalimbali. Alibainisha kuwa mfumo huo hauishii katika uwezo wa kijeshi pekee, bali pia unahusisha vipengele vya kitamaduni, kijamii na kimedia, ambavyo vina mchango mkubwa katika kuimarisha uwezo wa taifa kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Your Comment