13 Juni 2026 - 16:41
Ratiba ya Hafla za Kuaga na Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu Yatangazwa

Ratiba rasmi ya hafla za kuaga, kuswaliwa na mazishi ya kiongozi shahidi wa Umma wa Kiislamu imetangazwa, huku shughuli hizo zikitarajiwa kufanyika katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ratiba rasmi ya hafla / marasimu za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu imetangazwa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, siku za Jumamosi, tarehe 4 Julai 2026 (19 Muharram 1448 H) na Jumapili, tarehe 5 Julai 2026 (20 Muharram 1448 H) zitafanyika hafla za kuaga mwili wa marehemu katika Msikiti wa Swala za Ijumaa wa Imam Khomeini (q.s.) mjini Tehran.

Siku ya Jumatatu, tarehe 6 Julai 2026 (21 Muharram 1448 H) kutafanyika hafla rasmi ya mazishi katika mji wa Tehran, ambapo waombolezaji na wananchi wanatarajiwa kushiriki kwa wingi.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa siku ya Jumanne, tarehe 7 Julai 2026 (22 Muharram 1448 H) mazishi yataendelea katika mji mtukufu wa Qom.

Aidha, siku ya Alhamisi, tarehe 9 Julai 2026 (24 Muharram 1448 H), inayosadifiana na mkesha wa kumbukumbu ya shahada ya Imam Zayn al-Abidin (a.s.), hafla ya mwisho ya mazishi itafanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad, ambapo mwili wa marehemu utazikwa katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (a.s.).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha