13 Juni 2026 - 17:03
Mohsen Rezaei: Trump Amekubali Kuachia Dola Bilioni 24 za Mali za Iran Zilizokuwa Zimezuiwa

Mwanachama wa Baraza la Kutambua Maslahi ya Taifa la Iran, Jenerali Mohsen Rezaei, amesema Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuachia dola bilioni 24 za mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa, ingawa hataki kutangaza uamuzi huo hadharani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jenerali Mohsen Rezaei, aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wakati wa Vita vya Kujihami Vitakatifu (1980–1988) na ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Baraza la Kutambua Maslahi ya Taifa la Iran, amesema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuachia dola bilioni 24 za mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa.

Rezaei alitoa kauli hiyo Ijumaa jioni wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuuawa shahidi kwa Jenerali Gholam Ali Rashid, aliyekuwa Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s.a.w.), pamoja na mwanawe, Hujjatul-Islam Mohammad Amin Rashid, katika hafla iliyofanyika katika Husseiniya ya Tharullah mjini Dezful, mkoani Khuzestan, kusini-magharibi mwa Iran.

Alisema kuwa, licha ya Trump kukubali kuachia mali hizo za Iran, hataki kulitangaza suala hilo waziwazi mbele ya umma.

Aidha, Rezaei alisisitiza kuwa uimara wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nguvu zake za kijeshi umeifanya Marekani kubadili msimamo wake, akidai kuwa hali hiyo imemfanya Trump kuwa mwangalifu zaidi katika kushughulikia mazungumzo na Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha