Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Seyyed Abbas Araghchi, ametoa salamu za rambirambi na pole kwa Serikali na wananchi wa Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo la Amerika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Araghchi alipiga simu kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiboivaria ya Venezuela, Ivan Gil Pinto, ambapo alieleza masikitiko ya Serikali na wananchi wa Iran kutokana na maafa hayo ya asili yaliyosababisha madhara makubwa.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika alasiri ya Jumamosi, mawaziri hao wawili walibadilishana maoni kuhusu athari za janga hilo, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akitangaza utayari wa Tehran kushiriki katika operesheni za uokoaji, utafutaji na utoaji wa misaada kwa waathirika wa tetemeko hilo.
Araghchi alisisitiza mshikamano wa Iran na taifa la Venezuela katika kipindi hiki kigumu, akieleza matumaini yake kwamba juhudi za pamoja za uokoaji na misaada zitasaidia kupunguza mateso ya waathirika na kuharakisha kurejea kwa hali ya kawaida nchini humo.
Your Comment