Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain, Ayatullah Sheikh Isa Ahmad Qassim, ametoa taarifa ya rambirambi kufuatia kuaga dunia kwa Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akimtaja kuwa alikuwa mwanamapinduzi aliyejitolea kwa ajili ya Uislamu, Umma wa Kiislamu na ubinadamu.
Katika ujumbe wake uliotolewa sambamba na shughuli za kuaga na mazishi ya kiongozi huyo, Sheikh Isa Qassim alisema kuwa mamilioni ya waombolezaji kutoka Iran na mataifa mbalimbali ya dunia wameungana kumuaga mwanazuoni mkubwa, faqihi, mwanasiasa mwenye busara na kiongozi mwaminifu aliyekuwa mfano wa ucha-Mungu na kujitolea katika kuitumikia dini.
Alisema kuwa uongozi wa Imam Ruhollah Khomeini na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei umefungua milango ya kheri kwa ulimwengu na kufunga milango ya maovu, akisisitiza kuwa jamii ya wanadamu itanufaika kwa kurejea katika mafundisho ya Uislamu wa kweli na uongozi unaozingatia misingi ya Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume Muhammad (SAW) pamoja na Ahlul-Bayt (as).
Sheikh Isa Qassim alieleza kuwa viongozi hao wawili waliiongoza Iran kurejea katika njia ya Uislamu halisi na kwamba mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ni matokeo ya uongozi uliojengwa juu ya imani, hekima na kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Aidha, alitoa dua ya kuiombea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Muqawama wa Kiislamu na Umma wa Waumini kuendelea kuwa thabiti katika njia ya haki, akiomba Mwenyezi Mungu awajaalie ushindi na kuharakisha faraja ya Imam Mahdi (af).
Your Comment