Kwa mujibu wa shirika la habari la Abna kwa kunukuu Al-Mayadeen, Mohammed Abdus-Salam, mkuu wa kamati ya mazungumzo ya Sanaa, alisisitiza: Uvamizi dhidi ya uwanja wa ndege wa Sanaa uliwakumbusha wale waliosahau kwamba Saudi Arabia inasisitiza kufungwa kwa uwanja huu wa ndege. Riyadh, kwa kutoa taarifa, inadai kwamba lengo lake ni kulinda uhuru wa Yemen.
Aliongezea: Ni kwa kiasi gani tabia za Saudi Arabia katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na uwongo, uadui na uvamizi, zinafanana na Israel. Kujificha nyuma ya taarifa zisizo za haki za Umoja wa Mataifa, ambazo zinotolewa kwa msingi wa uhusiano wa mafuta na Saudi Arabia, haziwezi kuficha ukweli wa mzingo usio wa haki dhidi ya Yemen. Saudi Arabia iko nyuma ya mzingo huu usio wa haki; nchi mvamizi ambayo ilianzisha vita vya miaka 8 dhidi ya Yemen na hatimaye ikashindwa, sasa inatafuta kufidia hasara.
Abdus-Salam alisisitiza: Kile ambacho Saudi Arabia inapaswa kuzingatia katika kipindi hiki ni kwamba, kwa makosa ya hesabu, imejigeuza kuwa adui wa wazi wa Yemen. Kusisitiza kwa Saudi Arabia kwenye ukaidi na kukataa kukubali ukweli, kutakuwa na matokeo makubwa kwa nchi hii, usalama wake na uchumi wake. Mzingo wa baharini ni hatua ya kwanza katika vita ya «mzingo dhidi ya mzingo», na watu wetu watapata haki zao.
Maoni yako