19 Machi 2011 - 20:30

Abna inatuarifu kuwa:Rais Barack Obama wa Marekani kwa mara nyingine tena ameudhihirishia ulimwengu jinsi utawala wa Washington ulivyojengeka juu ya misingi ya dhulma na unafiki baada ya kurefusha kwa mwaka mmoja zaidi vikwazo dhidi ya Sudan.

Tangazo la Rais Obama ni kinyume na ahadi yake ya huko nyuma kwamba vikwazo dhidi ya Sudan vingefutwa kama Khartoum ingeruhusu kufanyika kura ya maoni kuamua hatma ya Sudan Kusini. Licha ya serikali ya Sudan kuruhusu kura hiyo kufanyika kwa njia ya amani na uwazi na hatimaye kujitenga Sudan Kusini, lakini Rais Obama amesema sera za Khartoum hazijabadilika na kwa mantiki hiyo vikwazo vya Washington dhdi ya Khrtoum vitaendelea kuweko kwa mwaka mwingine zaidi. Vikwazo hivyo vya kibiashara viliwekewa Sudan tangu mwaka 1997.