Ripoti ya ABNA- Maandamano hayo yamefanyika pia katika miji ya Karak, Maan na Tafileh. Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan amelazimika kuwauzulu Mawaziri Wakuu wawili ili kuzuia upinzani zaidi dhidi ya serikali yake kufuatia maandamano makubwa ya wananchi. Wananchi wa Jordan tangu mwezi Januari mwaka huu wamekuwa wakiandamna kutaka mabadiliko nchini humo na mwezi Juni, Mfalme Abdullah wa Pili alitangaza kukubali kuundwa serikali mpya itakayochaguliwa na wananchi badala ya kuteuliwa na mfalme. Hata hivyo baadaye alisema kuwa itachukua miaka miwili hadi mitatu kuweza kutekelezwa jambo hilo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 276559
Mamia ya wananchi wa Jordan wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Amman wakitaka serikali mpya ya nchi hiyo itekeleza ahadi zake za kuleta mageuzi na kupambana na ubadhirifu. Waandamanaji hao walioandamana baada ya sala ya Ijumaa ya jana wamemtaka Waziri Mkuu Awn al Khasawneh kuyapa kipaumbele cha kwanza mageuzi ya kisiasa.