19 Machi 2011 - 20:30

Mustapha Abdul Jalil, Mkuu wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya yuko nchini Sudan kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Khartoum

Abdul Jalil jana Ijumaa aliwasili Khartoum kwa ajili ya ziara ya siku mbili inayohesabiwa kuwa ya kwanza nchini humo, kufanywa na kiongozi wa ngazi za juu wa Libya baada ya kuanguka utawala wa Muammar Gaddafi. Abdul Jalil alilakiwa na Rais Omar al Bashir wa Sudan, Waziri wa Mawasiliano wa nchi hiyo, Kamal Abidi na msemaji rasmi wa serikali ya Khartoum ambapo viongozi wa nchi hizo mbili wamejadiliana umuhimu wa kustawishwa uhusiano wa pande mbili. Uhusiano wa Sudan na Libya haukuwa mzuri wakati wa utawala wa Gaddafi kwa sababu kiongozi huyo wa zamani wa Libya alikuwa akidaiwa kuwasaidia waasi wa eneo la Darfur na Sudan Kusini iliyojitenga mwezi Julai mwaka huu. Baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwa, safari ya Abdul Jalil nchini Sudan imefanywa kwa lengo la kuishukuru nchi hiyo kwa kuwasaidia kisilaha wananchi wa Libya zilizowasaidia wanamapinduzi kuupinduliwa utawala wa Gaddafi.