19 Machi 2011 - 20:30

Maafisa wa Libya wameainisha muhula wa kuwapokonya silaha wakazi wa Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo kuwa ni hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu na kuvitaka vikosi vya wanamapinduzi kutoka nje ya mji huo viwe vimeshaondoka Tripoli ifikapo tarehe 20 Disemba.

Maafisa wa Libya wameainisha muhula wa kuwapokonya silaha wakazi wa Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo kuwa ni hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu na kuvitaka vikosi vya wanamapinduzi kutoka nje ya mji huo viwe vimeshaondoka Tripoli ifikapo tarehe 20 Disemba. Serikali ya Libya imeunga mkono kwa dhati muhula huo wa wiki mbili uliotolewa kwa vikosi vya wanamapinduzi kuondoka huko Tripoli. Abdulrahim al Kib Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Libya amesema kuwa wananchi watakusanyika leo katika maidani ya mashahidi katika juhudi za kuunga mkono hatua ya serikali ya kuuweka mji wa Tripoli pasina silaha na wanamgambo wasio na ulazima.