19 Machi 2011 - 20:30

Maandamano ya wananchi wa Saudi Arabia dhidi ya utawala wa kifalme nchini humo yameendelea hata baada ya vikosi vya usalama kuwaua shahidi waandamanaji kadhaa.

Katika mahojiano na Press TV, Ali Al Ahmad, mtaalamu wa masuala ya kisiasa ameashiria machafuko katika miji ya Saudia Arabia kama vile Qatif na Awamiya na kusema watawala wa nchi hiyo wameingiwa na wasi wasi mkubwa kwani maandamano hayo yamkini yakafika katika mji mkuu Riyadh. Mtaalamu huyo ametoa wito kwa wananchi wa Saudi Arabia kuungana katika mapambano yao dhidi ya watawala wa kifalme nchini humo ambao ni vibaraka wakubwa wa Marekani. Ali al Ahmad amesema kuna mwamko mkubwa wa Kiislamu nchini Saudia na kwamba walio wengi wanataka mabadiliko ya kimsingi.