Mamia ya wananachi wanamapinduzi nchini Misri wanaoendelea kuandamana katika medani ya Tahrir mjini Cairo kupinga Baraza la Kijeshi, wamekimbizwa hospitalini baada ya kutiliwa sumu katika vipande vya mkate vyenye nyama. Shirika la Habari la Misri Mena limeripoti kuwa, mwanamke mmoja aliyekuwa amejifunika uso alishuka kutoka garini na kupeana vipande hivyo vya mkate vilivyotiwa sumu kwa waandamanaji na kisha kutoweka. Baadhi ya waandamanaji waliokula mikate hiyo walianguka chini na kuziraia huku wengine wakitapika na kutokwa na majasho kabla ya kukimbizwa hospitalini. Walioshuhudiwa kisa hicho wanaamini kuwa, huenda hiyo ni njama iliyopangwa na mabaki ya walioukuwa wakiunga mkono utawala wa kidikteta wa Husni Mubarak. Tangu mwishoni mwe mwezi uliopita, wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana dhidi ya Baraza la Kijeshi linalotawala Misri sasa.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 284237
Mamia ya wananachi wanamapinduzi nchini Misri wanaoendelea kuandamana katika medani ya Tahrir mjini Cairo kupinga Baraza la Kijeshi, wamekimbizwa hospitalini baada ya kutiliwa sumu katika vipande vya mkate vyenye nyama.