Wafanyakazi wa utoaji misaada wamesema kuwa, waasi hao wanadai kuwa wanataka kuangalia ubora wa chakula hicho, lakini shirika hilo lina wasiwasi kuwa kundi hilo linatafuta kizingizio cha kupiga marufuku shughuli zake za kutoa misaada kama lilivyofanya kwa mashirika mengine.Licha ya hatua hiyo msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu mjini Geneva Nicole Engelbrecht amesema, oparesheni za shirika hilo za kutoa misaada zinaendelea Somalia huku majadiliano yakifanywa kati ya pande mbalimbali kuhusiana na suala hilo.Waasi wa as Shabab wanaodhibiti maeneo mengi ya Somalia kipindi cha nyuma walipiga marufuku misaada ya chakula lakini baadaye waliondoa marufuku hiyo. Wananchi wengi wa maeneo ya kusini mwa Somalia wanahitajia misaada ya chakula kutokana na njaa na ukame.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 284443
Wanamgambo wa kundi la as Shabab la Somalia wamezuia msafara wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu uliokuwa umebeba misaada ya dharura ya chakula kwa ajili ya watu wanaosumbuliwa na njaa kutokana na ukame nchini humo.