Wanajeshi wasiopungua watano wa serikali ya mpito ya Somalia na wapiganaji 13 wa al Shabab wameuawa katika ufyatuaji risasi kati ya pande mbili hizo huko kusini mwa Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo. Afisa wa jeshi la Somalia katika kituo cha kijeshi cha Gashandhiga ameeleza kuwa mauaji hayo yametokea mapema leo katika mtaa wa viwanda kusini mwa Mogadishu baada ya wapiganaji wa al Shabab kuzishambulia kambi za vikosi vya Umoja wa Afrika na serikali ya Somalia.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 285077
Wanajeshi wasiopungua watano wa serikali ya mpito ya Somalia na wapiganaji 13 wa al Shabab wameuawa katika ufyatuaji risasi kati ya pande mbili hizo huko kusini mwa Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo