19 Machi 2011 - 20:30

Balozi wa Misri nchini Marekani ametoa wito kwa serikali ya Washington akiitaka izuie mali za shaksia 100 waliohudumu katika serikali iliyoanguka ya Hosni Mubarak.

Balozi wa Misri nchini Marekani ametoa wito kwa serikali ya Washington akiitaka izuie mali za shaksia 100 waliohudumu katika serikali iliyoanguka ya Hosni Mubarak. Sameh Shukri amesema watu hao wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na utumizi mbaya wa madaraka na kwa mantiki hiyo, Marekani inapaswa kuzuia mali zao. Utawala wa miaka 30 wa Hosni Mubarak ulianguka Februari 25 mwaka huu baada ya maandamano ya majuma kadhaa ya wananchi katika miji yote ya Misri huku shina la maandamano hayo likiwa medani ya Tahrir mjini Cairo.