19 Machi 2011 - 20:30

Kundi la Ikhwanul Muslimin nchini Misri limesema kuwa, kamwe haliwezi kuitambua Israel.

Bw. Rashad al Bayoumi, kiongozi nambari mbili wa kundi hilo lenye ushawishi mkubwa nchini Misri amesema hayo na kuongeza kuwa, mikataba yote iliyotiwa saini huko nyuma kati ya Cairo na Tel-Aviv ukiwemo ule wa amani itawekwa mbele ya wananchi wa Misri waamue cha kufanya.Chama cha Ikhwanul Muslimin ndicho kinachoongoza kwa viti vingi katika uchaguzi wa Bunge ulioingia kwenye awamu yake ya mwisho nchini Misri.Bw. Bayoumi ameongeza kuwa, serikali mpya itakayoingia madarakani nchini Misri haitajali nini kitatokea baadaye. Amesema, Ikhwanul Muslimin kamwe hawawezi kuitambua Israel, kwani ni adui nambari moja wa Waislamu na ambaye anazikalia kwa mabavu ardhi kadhaa za Waislamu.Amesema, kamwe hawezi kuiruhusu nafsi yake kukaa meza moja na maadui na watenda jinai kama viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.