Shambulizi hilo limetokea katika jimbo la Adawama. Mashambulizi kama hayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara pia dhidi ya Waislamu nchini humo.Hali ni mbaya nchini Nigeria kiasi kwamba siku ya Jumamosi, Rais Goodlack Jonathan wa nchi hiyo alitangaza hali ya hatari katika juhudi za kujaribu kudhibiti hali ya mambo na kuzima mashambulizi ya watu wenye silaha.Machafuko na mashambulizi yanayolenga makundi ya Waislamu na Wakristo nchini Nigeria yameongeza wasiwasi wa kushadidi mgogoro kati ya jamii za makundi hayo mawili nchini humo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 289140
Watu wasiopungua 20 wameuawa baada ya mtu mmoja mwenye silaha kushambulia jumba la mikutano huko kaskazini mwa Nigeria kulikokuwa kukifanyika mkutano wa kundi la Kikiristo la Igbo.