19 Machi 2011 - 20:30

ABNA inatuarifu kuwa:Maofisa wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wamesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wamepata mapendekezo mapya ya hatua za kuchukua dhidi ya Syria.

Mapendekezo hayo mapya yanakuja ikiwa siku ya Jumatatu imeshuhudiwa wajumbe wa Baraza la Usalama wakishindwa kukubalina kwa kauli moja kuhusu hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya serikali ya Syria.Mapendekezo hayo mapya ambayo yanalenga kuweka vikwazo vya hali ya juu dhidi ya Syria  na kutaka serikali ya rais Asad Kujiuzulu.

ni mpango ulipendekezwa na mataifa ya magharibi na kuungwa mkono na Umoja wa nchi za Kiarabu, Marekani, Ufaransa na Uingereza ulipingwa vikali na nchi za Urusi pamoja na China.yafaa kuashiria kwamba nchi za magharibi zimekuwa zikifumbia macho baadhi ya mauaji yanayofanywa na baadhi ya nchi zenye uhusiano nazo na badala yake kukuza na kusambaza habari za urongo kwa nchi mahasimu wao jambo ambalo linapingwa vikali na nchi mfano wa China na Urusi.

Urusi imeendelea kushikilia msimamo wake wakutochukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria wala kuweka vikwazo vigumu zaidi kwa nchi hiyo ikisema kuwa kufanya hivyo kutasababisha nchi hiyo kutumbukia katika vita za wenyewe kwa wenyeweKufuatia hatua hiyo nchi ya Urusi imesema kuwa itatumia kura yake ya turufu kupinga mpango wowote wa Umoja huo kutaka kutumia nguvu dhidi ya serikali ya Syria, hatua mabayo imeungwa mkono na China