19 Machi 2011 - 20:30

Mfalme wa Bahrain katika maneno yake ya kudhihaki Wanawake alisema kuwa Nchi ya Bahrain imejiandaa kiukamilifu katika kuhami Wanawake.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Sheikh Hamad Ibn Issa Alikhalifa  katika maongezi yake na Shpighel alidai kuwa wapinzinai wanajitahidi kuharibu umoja wa Nchi.

Akiendelea kusema katika kupingwa waandamanaji wanaopinga Serikali katika mwaka huu na mwaka uliopita alieleza kua; tumejiandaa ukamilifu kwa lengo la kuhami Wanawake na Wanawake wanaoandamana katika Nchi si Wanawake wa Bahrain ni Wanawake kutoka nje ya Bahrain walokuja kuharibu umoja wa Wananchi wa Bahrain.

Maneno haya ni ya kuwadhihaki Wanawake na kuafanyia masihara, sivyo tu bali pia maneno hayo ni ya  kuchekesha kwani sote tumeshuhudia mwaka ulopita na mwaka huu  ni kiasi gani vyombo vya usalama vya utawala wa Bahrain vinawapiga  na kuwakandamiza Wanawake na kutotosheka na matendo yao wanawavulia heshima Wanawake wanaoandamana na kupinga utawala wa Alikhalifa.

Sheikh Hamad Ibn Issa Alikhalifa pia alidai kuwa wameandaa vikosi vya kusaidia Wanawake wakisaidiana na umoja wa Persian Gulf, na pia kuandaa vikosi vya usalama kwa lengo kuzuiya maadui wa Nchi akimaanisha adui huyo ni ni Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran.