19 Machi 2011 - 20:30

Baadhi ya Waumini wa kiislamu wafanya Sherehe za kumkirimu Mama mmoja wa Bulgaria kwa kukubali kwake Uislamu kuwa Dini yake, sherehe hiyo ilifanyika Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Irani Nchini Bulgaria.

Ripori ya shirila la habri la Ahlul Bayt(as)-ABNA- katika kuendeleza Tamaduni za Kiislamu Duniani na athari za Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Bulgaria Mama mmoja baada ya kuathirika na Dini Uislamu hasa Madhehebu ya Shia alichagua Uislamu kuwa Dini yake.

Sherehe za kumkirimu Mama hyo wa Kibulgaria kwa kukubali kwake Uislamu kuwa Dni yake, na kuhudhuriwa sherehe hiyo na Balozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Bulgaria, na sherehe hiyo ilifanyika ndani ya Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Irani Nchini Bulgaria.

Katika sherehe hizo  Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jumuhuri ya Kiislamu ya Iran Bulgaria alihutubu akisema: sababu kuu ya  Mama huyu kuukubali Uislamu ni kuvutiwa na Madhehebu ya Shia na na ujumbe mzima alotuletea bwana Mtume Muhammad(s.a.w.w).

Akiendelea kusema; kukubali kwake Uislamu ni baada kuuliza na kujibiwa ndio alichua uwamuzi kukubali Uislamu na Madhehebu ya Shia.

Mama huyo pia alisema kuwa: kukubali kwangu Uislamu ni baada ya kuvutiwa na vitendo vya Mashia na msimamo wao  uliotofauti na Madhehebu mengine, hasa baada kuonekana kuwa Mshia ndio wapo dhidi ya Marekani na Maadui wa Uislamu kwa ujumla, suala hili lilinipelekea kufikiri sana na kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu, kwanini Mashia wakawa na misimamo imara kama hiyo na badala yake Masunni hasa Viongozi wa kisuni kuwa kimya na kuwa madhalili  mbele ya  Marekani na Maadui wa Uislamu?!

Mwisho wa sherehe hizo alipewa zawadi ya thamani isokuwa na kifani nayo Kitabu cha Mwenyezi Mungu QURANI TUKUFU.