Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA-Mama mwenye umri wa miaka 59 alifariki baada ya kushiriki katika maandamano ya kuutaka utawala wa Bahrain kujitoa madarakani, na uchunguzi umeeleza kuwa sababu ya kifo chake ni Gesi ya sumu inayotumiwa na Polisi Nchini humo.
Mama huyu alifariki katika Kijiji cha A`aliy, na kutoka katika Kijiji hicho kuelekea Mji Mkuu Manamah ni kilometa 3 tu.
Nchi ya Bahrain sasa imekabiliwa na msukumo mkali wa maandamano ya Wananchi kutaka kuondoa utawala wa Kifalme Nchini humo, utawala Nchi ndogo hiyo ilokuwepo katika maeneo ya Perian Gurf umeona kuwa hatua ya kuzuiya maandamano hayo ni kukandamiza Wananchi kushirikiana na viikosi haramu vya Saudia Arabia.
Maandamano ya Bahrain yalianza mnamo mwaka 2011 kupinga utawala wa kidikteta na kuutaka kuondoka haraka iwezekanavyo.
Utawala wa Alikhalifa kusaidiwa na Saudia Arabia waendelea kuuwa na kuwatendea Wananchi Bahrain kwa kosa la kuandamana dhidi ya utawala na kutaka kukubaliwa maombi yao, na kwa vitendo hivyo mamia ya watu wamejeruhiwa upelekwa Ospitalini na baadhi yao kufariki kabla ya kufika Ospitali.
Kwa vitendo vyote hivyo vyombo vya kutetea hali za binadamu vya Ulaya vipo kimya na kuunga mkono kile kinachofanywa na utawala wa Bahrain kushirikiana na Saudia Arabia.