21 Aprili 2012 - 19:30

Maelfu ya Wabahrain wameandamana katika kijiji kichokua karibu na mji mkuu wa Bahrain, Manama jana jioni kwenye uwanja unaofanyika mashindano ya magari ya Formula One.

Waandamanji hao walikusanyika kwenye eneo la Darraz umbali wa  kilometa 10 kutoka  kwenye  kituo cha mashindano hayo wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuupinga utawala wa Kifalme nchini Bahrain. Maandamano hayo yanayafuatia yale yaliyofanyika katika vijiji kadhaa vilivyo kuwa karibu na Manama ambapo polisi waliokuwa wakiyazuia walitumia mabomu ya machozi na ya sauti  kubwa ili kuwatawanya waandamanaji. Kikundi kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha Al-Wefaq, hapo awali kiliripoti kuhusu kifo cha mmoja wa waandamanaji. Mwili wa mtu  huyo  Salah Abbas Habib, ulikutwa katika kijiji cha Shakura. Polisi nchini huyo wamedai  kuanza uchunguzi kuhusu kuhusu kifo cha mtu huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama kushirikiana na Saudia Arabia.