Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Sheikh Omar Fustuq Kiongozi wa shirika la uhamiaji Uingireza aliseama: Mtuhumiwa wa mauaji ya Bulgaria ni Mahdi Ghazali mbaye alitega bomu katika Basi na kusababisha mauaji ya Waisraeli 6 walokuwa wakisafiri Nchini Bulgaria.
Akiendelea kusema: Wote wa fahamu kuwa Mahdi Ghazali ni mkazi wa Uingereza na anauhusiano na vikundi vya Itikadi kali Nchini, na katika Nchi hii kuna vikundi tofauti vya Jihadi na ikiwa mtuhumiwa ni Mahdi Ghazali vikundi hivyo vya jifaharisha kwa kitendo hicho.
Omar Bakri akiongea na Televisheni ya Al-Jadid alisema:Kama zisingelisambazwa picha hizo hatungelimfahamu na sisi hatumfahamu kwa jina la Mahdi Ghazali bali twamfahamu kwa jina la Abu Ahmad Maaruf na kwa mantiki hii hakuwa ni mkazi wa Uingereza wala hana hata karatasi za uhamiaji.
Abu Ahmad Maaruf ni mwenye asili ya Algeria na si kama inavyodai Viongozi wa Israel kuwa ni Muirani au ni mtu wa Kikundi cha Hizbullah Lebanon.