Bado sakata la tuhuma za baadhi ya wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), linazidi kugonga vichwa vya habari nchini humo, tena katika wakati huu ambapo inadaiwa vitendo vya rushwa vinaota mizizi katika kila nyanja. Mmoja kati ya waandishi wa habari alimuuliza Prof. Benson Bana, kutoka Idara ya taaluma ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwanza alimuuliza tuhuma hizo za rushwa kwa wabunge amezipokeaje?
Alijibu Prof. Benson Bana: Suala hili lasemwa na kuthibishwa na mashuhuda kuwa Wabunge wala Rushwa.