15 Agosti 2012 - 19:30

Mazishi ya miili ya mashahidi waliowawa katika jangwa la Sinaa yamepelekea kufichuka siri yakuwepo mpango wa kumuua Rais wa Jamhuri ya Misri

Vyombo vya habari vinanukuu kuwepo mpango wa kumuua Muhammad Mursiy Rais wa Jamhuri ya Misri katika mazishi ya mashahidi waliouwawa katika mpaka wa Rafah katika jangwa la Sinaa, aidha katika habari hizo pia imeashiria kuwpo maandalizi ya mapinduzi ya kijeshi kwa Rais wa nchi hiyo mwishoni mwa mwezi huu. Habari hii imetangazwa na kikundi cha masuala ya ulinzi nchini humo na ripoti kamai ya masuala hayo amekabidhiwa Rais huyo , na uhakika wa habari hiyo inaashiria vitisho vya wazi vya mpango wa mauaji hayo.